Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI Mh. James Mbatia
amesema endapo tume ya uchaguzi itaendelea na utaratibu uliotumika mkoani
njombe itatumia zaidi ya miaka 10 kuandikisha na kuongeza kuwa kwa sasa suala
la kura ya maoni liwekwe pembeni na serikali isitishe mambo yote yasiyokuwa ya
msingi ielekeze nguvu zake kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura
ili limalizike kwa wakati.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chadema Mh
Freeman Mbowe amesema hakuna mgawanyiko ndani ya ukawa licha ya kuwepo kwa
changamoto za hapa na pale na kwamba tayari wameshafanya mgawanyo wa majimbo
kwa asilimia 95 ambayo wamekubaliana isipokuwa majimbo 12 ambayo bado
wanavutana lakini bado wako kwenye masahauriano.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahimu Lipumba
amesisitiza kuwa UKAWA haiungi mkono jaribio lolote la kufanya marekebisho ya
katiba ya sasa kwa lengo la kuongeza muda wa utawala uliopo madarakani kwani
kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na katiba ya nchi na ukiukwaji wa
sheria huku akiitadharisha serikali
kutokuipeleka nchi kwenye machafuko yanayotokea burundi hivi sasa.
0 comments:
Post a Comment