Wakizungumza katika mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mazinde wilayani Korogwe
na kuhudhuriwa na wadau wa afya ngazi ya wilaya,viongozi wa
serikali na kamati ya ulinzi na usalama chini ya Mwenyekiti wake mkuu wa
wilaya hiyo wazee hao wamesema mbali na sera hiyo kupingwa,pia kadi
zao za uanachama wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) zinashindwa kutambuliwa
wanapokwenda kupata huduma katika kituo cha afya cha mombo na
hospitali ya wilaya ya korogwe.
Hata hivyo mwenyekiti wa bodi
ya afya wa wilaya ya korgwe Bwana Charles Gawile amewataka wananchi wa eneo
hilo kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa kwa viongozi wa bodi hiyo endapo kuna
hujuma za ubathirifu wa dawa zinazopelekwa katika zahanati ya kata yao
zinazosimaiwa na kamati ya afya ngazi za vijiji ili hatua kali za kisheria
ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Kufuatia hatua hiyo daktari
wa zahanati ya kata ya Mazinde ambayo imesajiliwa na mfuko wa afya ya
jamii Dr,Dunstan Wandi amesema malalamiko ya wananchi kuwa hawapati dawa
hayasababishwi na viongozi wa afya na badala yake unapoagiza dawa bohari
kuu ya dawa nchini (MSD) wanatekeleza baada ya miezi minne hatua ambayo
imesababisha kero na wananchi kukataa kujiunga na mfuko huo.
0 comments:
Post a Comment