Waziri wa ardhi,
nyumba na maendeleo ya makazi Mh.William Lukuvi amemuagiza mkurugenzi wa
halmashauri ya jiji la mwanza na manispaa ya ilemela kuwachukulia hatua za
kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani baadhi ya watendaji wa ardhi katika
halmashauri hizo wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya udanganyifu katika
umilikaji na ugawaji wa ardhi na kusababisha malalamiko 395 ya migogoro ya
ardhi.
Waziri Lukuvi
ametoa agizo hilo jijini mwanza wakati akipokea taarifa ya malalamiko kutoka
katika timu ya wataalam aliyoiunda mwezi mmoja uliopita ambapo amesema baada ya
uchambuzi wa kina kufanyika imebainika kuwa malalamiko 141 kati ya 395 yanahusu
fidia,70 yanahusu usimamizi duni wa kupanga, kupima na ugawaji wa ardhi, wakati
malalamiko 54 yanahusu uelewa mdogo wa kanuni, sheria na taratibu kwa watendaji
wa ardhi na wananchi na malalamiko 42 yanahusu uvamizi wa maeneo ya watu
binafsi na ya umma hasa kwenye vilima.
Mh. Lukuvi amesema
kwamba kwa wananchi ambao hawataridhika kabisa na hatua za serikali katika
kushughulikia malalamiko yao amewaelekeza cha kufanya.
Kuhusu baadhi ya
wenyeviti wa serikali za mitaa katika manispaa ya ilemela na jiji la mwanza
kujichukulia sheria mkononi na kuanza kugawa viwanja kwa wananchi - waziri huyo
mwenye dhamana ya ardhi amesema ni kosa kisheria na bila kutafuna maneno kibao
kikamgeukia mkurugenzi wa manispaa ya ilemela kwa kuvamia kiwanja cha mkazi wa
bwiru alichokuwa amepewa na idara ya ardhi ya manispaa hiyo.
0 comments:
Post a Comment