Image
Image

News Alert: ITV yashinda tuzo ya ubora SUPERBRAND Afrika Mashariki kwa mwaka 2015 na 2016 kundi la makampuni kumi bora katika tuzo hizo.


Kituo cha televisheni cha ITV kimeibuka tena kidedea mwaka huu na kujinyakulia tuzo ya ubora ya  supebrand afrika mashariki kwa mwaka 2015-2016 kikiwa ni kituo pekee cha televisheni  katika kundi la makampuni  kumi bora  katika tuzo hizo.
ITV na CLOUDS FM radio ndio makampuni pekee ya habari yaliyopata tuzo hizo  mwaka huu ambapo mara baada ya kupokea tuzo hiyo, mkurugenzi mtendaji wa ITV RADIO ONE Joyce Mhaville mbali na kuwashukuru wateja na jamii kwa ujumla  amesema tuzo hiyo ina maana kubwa kwa kampuni yake  ambayo tayari imechomoza kwenye soko la Afrika mashariki ikijipanga  kujikita kwenye soko la Afrika kwa ujumla.

Mkuu wa idara ya uchunguzi wa viwango SUPERBRANDS Afrika Mashariki Bw.Jawad Jaffer  amesema tuzo hizo zimezingatia maoni ya wataalam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma na bidhaa huku akivishukuru vyombo vya habari nchini kwa kuwezesha waandaaji kuzitangaza bidhaa na makampuni ya kitanzania na kuipongeza ITV kwa kuendelea kufanya vizuri.
 Mkurugenzi mtendaji wa ITV RADIO ONE Joyce Mhaville.
Kwa upande wao baadhi ya washindi wengine wamesema tuzo hizi zinaonyesha kuaminika na kukubalika kwa huduma zinazotolewa na makampuni yao na kuwa changamoto kwao kuhakikisha wanaboresha zaidi huduma zao.
Zaidi ya makampuni 1000 yalipambanishwa kwa kufanyiwa utafiti wa kina na kisha kubaki makampuni 20 pekee huku jumla ya kampuni 11 zinazotoa huduma za kuzalisha bidhaa zikiendelea kung'ang'ania kwenye orodha ya 20 bora ya SUPERBRANDS.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment