Akiwasilisha mapendekezo ya mfumo
wa mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka 2015/16 kwa wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,
waziri wa fedha na uchumi Mhe.Saada mkuya amesema kati ya fedha hizo serikali
itatenga shilingi trilioni 16 na bilioni 711.2 kwa ajili ya matumizi ya
kawaida, shilingi trilioni 6 na bilioni 612 kwa ajili ya mishahara taasisi na
watumishi wa serikali ambapo fedha na miradi ya maendeleo imetenga shilingi
trilioni 5 na bilioni 769.2 sawa na asilimia 25 ya bajeti yote.
Awali akisoma mpango wa maendeleo
wa taifa kwa mwaka wa fedha 2015/16 waziri nchi ofisi ya Rais uratibu na
mahusiano,Mhe Dkt Mary Nagu amesema katika mwaka wa fedha 2015/16 makadirio ya
mahitaji ya fedha za kugharamia miradi ya maendeleo ni shilingi trilioni 6 na
bilioni 279 ambapo shilingi trilioni 4 na bilioni 838 ni fedha za ndani na
shilingi trilioni 1 na bilioni 441 ni fedha za nje na kusisitiza sehemu kubwa
ya fedha hizo zimeelekezwa katika maeneo ya kipaumbele ya miundombinu,kilimo,viwanda,elimu,afya
na maji.
Wakichangia mapendekezo hayo
baadhi ya mabunge wamesema hayalengi kumletea maendeleo mwananchi wa kawaida
changamoto zinazomkabili na hakuna unafuu wowote kwa kuwa imejikita zaidi
kutegeme vyanzo katika halmashauri
ambapo huko hakuna uwekezaji wowote, huku wengine wakitaka serikali kuwekeza
zaidi katika sekta ya utalii baada ya kuonekana kwa miaka miwili mfulilo
kuongoza katika kuiingiza taifa kimapato.
0 comments:
Post a Comment