Licha ya kupazwa sauti na wadau mbali mbali kila
kukicha juu ya kutafuta mwarobaini wa kuweza kumaliza ajali za bara barani ama
kupungua kabisa bado hali inaonekana kuchafuka kila baada ya iitwayo leo wimbo
uliotawala midomoni mwa wananchi ni neon Ajali ili hali tukiwa mimi nawewe
tukijiuliza Ajali ni nani,anatoka wapi,ni mtu ama upepo,ama nini ni haswa
tusemapo ajali?.
Wakati kila mmoja wetu akitafakari hilo bhasi punde
si punde navuta pumzi nasikia kama sauti ya kitu masikioni mwangu ambapo
nilipokea ujumbe mfupi wa maandishi ukisema Watu kumi na tano
wamejeruhiwa na wengine zaidi ya hamsini wakinusurika kufa baada ya basi la
kampuni ya TAKBIR Lililokuwa likitokea mkoani geita kuligonga basi la
kampuni ya ABOOD,maeneo ya Lubungo Mikese katika barabà ra kuu ya Morogoro-Dar
es Salaam.
Idadi hiyo ya manusura bado ingali ikiturudisha
nyuma kutafakari huyu aitwaye ajali ni nani?,wapo waliofunga, kusali na kuomba
na hata kulazimika kukusanyika kwenye nyumba zao za ibada kumuombea huyu ajali
atafunaye maisha ya watanzania kila itwapo leo bila huruma yoyote.
Ajali hii ambayo si nzuri imehusisha basi aina
ya SCANIA,mali ya kampuni ya TAKBIR lenye namba za usajili T.230 BRG,lililokuwa
likitokea mkoani Geita, kuelekea jijini Dar es Salaam, likiendeshwa na
PROJETUS MODESTUS, mkazi wa mabatini mwanza ambalo kwa mujibu wa mashuhuda wa
ajali hiyo,limeligonga kwa nyuma basi la kampuni ya ABOOD lililokua
likitokea Morogoro kuelekea Dar es Salam likiendeswa na Abdala Hemed, mkazi wa
kiwanja cha ndege Morogoro na kusababisha idadi hiyo ya majeruhi,wakiwemo
wanawake wanane, wanaume watano pamoja na watoto wawili,huku dereva wa TAKBIR
akidaiwa kukimbia baada ya ajali.
Nao majeruhi wa ajali hiyo wamebainisha chanzo cha
ajali ni dereva wa basi hilo kutokua makini na kuendesha gari kwa
mwendokasi,na kwamba wanashukuru wanaendelea na matibabu, huku kamanda wa
polisi mkoa wa morogoro Leonard Paulo akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na
kutoa wito kwa madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kutambua kuwa
wanabeba roho za wananchi na hatma ya roho hizo iko mikononi mwao.
0 comments:
Post a Comment