Image
Image

Wakazi wa kitongoji cha KITAME katika halmashauri ya wilaya ya BAGAMOYO washauriwa kutowakataa wawekezaji.


Wakazi wa kitongoji cha KITAME katika halmashauri ya wilaya ya BAGAMOYO mkoani PWANI wameshauriwa kutowakataa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika miradi mikubwa ya kuzalisha chuvi katika kitongoji hicho.
Ushauri huo umetolewa na Katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Mkombozi JUMANNE SALUM na kuongeza kuwa miradi hiyo itaharakisha kitongoji hicho kupata maendeleo.
SALUM ametoa ushauri huo alipowatembelea wakazi wa kitongoji hicho cha KITAME kwa lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kutambua na kutumia fursa zilizopo mkatika maeneo yao ili kujiletea maendeleo.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho cha KITAME wamekiri kuwa tayari wameanza kunufaika na miradi mikubwa ya kuzalisha chumvi kwa kuwa wawekezaji wachache walioanza kuwekeza wamewajengea shule na nyumba za walimu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment