Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa amri kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na makamanda wa meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.
PICHA NA IKULU.Na.Semvua Msangi,Dar es Salaam.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua meli mbili kubwa za kisasa za
kivita zenye meta 60, mizinga mikubwa miwili na ya kawaida sita kila moja, na
uwezo wa kupiga makombora umbali wa kilometa saba angani na kilometa tisa chini
ambazo zitakazowezesha usalama wa uhakika katika ukanda wa bahari wa tanzania
dhidi ya maharamia.
Mara baada ya uzinduzi Rais. Kikwete
amezikabidhi kwa kamandi ya jeshi la wanamaji hafla iliyofanyika makao makuu ya
kamandi hiyo yaliyopo kigamboni jijini Dar es salaam ambapo amesema meli hizo
zinafanya Tanzania iandike historia mpya ya kuwa na meli kubwa na za kisasa kwa
mara ya kwanza nchini.
Akizungumza katika uzinduzi huo
waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa,Dk.Hussein Mwinyi, amesema, meli
hizo zitakuwa tegemeo kubwa katika kulinda eneo la maji ya tanzania na
rasilimali zake ikiwamo gesi asililia,samaki kwani zina uwezo wa kasi kubwa
katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hasa uharamia.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi na
usama nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, amesema,lengo la kuwa na meli za
jinsi hiyo ni katika jitihada za kuhakikisha jeshi linakuwa na silaha za kisasa
za kivita na kutoa mafunzo huku balozi wa china nchini, Lui Youging,
akimpongeza Rais Kikwete kwa jitihada za kuimarisha ulinzi wa taifa lake.
Meli hizo zimepewa majina ya
melivita P77 Mwitongo kuwakilisha eneo alilozaliwa kiongozi wa kwanza wa
Tanzania, hayati Julius Nyerere na
melivita P78 Msoga, eneo alilozaliwa Rais Kikwete ambaye anatarajia kumaliza
kipindi chake cha uongozi Novemba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment