Kamati ya Bunge ya uchumi viwanda na uchumi imeitaka serikali kutoa
majibu kwa nini imepuuzia maagizo ya kamati hiyo hali ambayo imesababisha dola
ya marekani kupanda na kufikia 2025 kutoka 1650 miezi mitatu iliyopita.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa kamati hiyo Luhaga mpina
amesema walitoa maagizo mengi kwa serikali ambayo yamepuuzwa hivyo siku ya
alhamisi watatakiwa kuonana na kamati hiyo na kueleza kwa kina kuhusiana
na hali ya uchumi ilivyo hapa nchini.
Kwa upande wake waziri kivuli wa
fedha James Mbatia amesema madhaifu yaliyopo nchini ikiwemo uingizwaji wa
baadhi ya vifaa na vyakula vinavyoweza kupatikana hapa nchini navyo vimechangia
hali hiyo hivyo ni bora taasisi ama watu wanaoagiza vitu ama vyakula kutoka nje
ya nchi wakaacha kufanya hivyo.
Naye mkurugenzi mtendaji wa
taasisi ya sekta binafsi nchini -TPSF Geofrey Simbeye amesema waliitahadharisha
mapema benki kuu kuhusiana na mwenendo wa dola na kusema kuwa hali ilivyo sasa
ni bora zikafanyika jitihada za dharura kuinusuru.
Juhudi za kuwapata viongozi wa
benki kuu kuzungumzia kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola
ya marekani inaedelea licha ya kushindikanika kwa siku tano mfululizo kwa madai
kuwa wasemaji wa jambo hilo wapo katika vikao.
0 comments:
Post a Comment