Image
Image

Tume ya uchaguzi yaanza kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa BVR mkoani Iringa.


Licha ya kuonekana kusuasua uandikishwaji wananchi katika daftari la wapiga kura hatimaye tume ya uchaguzi imeanza kuandikisha wapiga kura katika daftari hilo kwa mfumo wa kielektroniki yaani  (BVR) mkoani iringa huku viongozi wa vyama vya CCM na CHADEMA  wakiitaka manispaa ya iringa kuongeza matangazo kuhamasisha wananchi kujitokeza zaidi.
Baadhi ya vituo vya uandikishaji vilivyoanza kazi hiyo hii leo ambapo kata tano za kitwiru,ruaha,igumbilo,nduli na mkimbizi zimefungua zoezi hilo litakaloendelea kwa siku saba kila kata na kukutana na viongozi hao wa kisiasa waliokuwa wanapita kukagua maendeleo ya zoezi hilo na kueleza kuwa mwitikio ni mzuri kwa siku ya kwanza.
Akizungumzia zoezi hilo afisa uchaguzi Bwana. Gabrial Msunza amesema manispaa hiyo yenye jumla ya vituo vya uandikishaji 192 katika kata 21 limegawanywa katika awamu nne na litamalizika siku ya tarehe 30 mwezi wa tano huku afisa habari wa manispaa hiyo bibi sima Bingileki akieleza kuwa manispaa hiyo inaendelea kufanya matangazo ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa kutumia njia mbalimbali hivyo hakuna haja ya wadau wa zoezi hilo kuwa na wasi wasi.
Zoezi hilo la uandikishaji wapiga kura linaendelea katika halmashauri zote nne za mkoa wa iringa ambapo viongozi wa serikali pamoja na vyama vya siasa wameendelea kuwasihi wananchi wa mkoa huu kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ambapo katika siku hii ya kwanza kasoro nyingi zilizoonekana awali wakati wa zoezi hilo mkoani njombe zimeonekana kudhibitiwa na tume ya taifa ya uchaguzi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment