Wanachama waliorudisha kadi ni wale wa Kijiji cha Kilewani,
wilayani humo, ambao walifanya hivyo katika mkutano wa hadhara wakati mbunge
huyo alipokuwa akihutubia kabla ya kukabidhi magari hayo kwa uongozi wa
halmashauri ya wilaya hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama hao walisema lengo lao
siyo kushabikia siasa bali kumuunga mkono mtu yeyote anayeweza kuwaletea
maendeleo kama alivyofanya mbunge huyo.
Monica Sichalwe, alisema
wameamua kurejea CCM kwa vile wanawake wilayani humo wamenyimwa nafasi ndani ya
Chadema.
Awali akiwapokea wanachama hao, Mbunge Kandege alisema wote wanaojeruhiwa na vyama vya siasa wanakaribishwa CCM kwani huko ndiko uliko uhuru wa kweli na demokrasia.
Alisema wanachama hao na viongozi walioamua kurejea CCM wamepokelewa kwa mikono miwili na kamwe hawatajutia uamuzi wao.

Kwa upande wake, Katibu
Mwenezi wa CCM wilaya ya Kalambo Leopard Mbita alisema wakati huu CCM haipo
tayari kuwafumbia macho wanachama na viongozi wake ambao ni tatizo hasa wakati
wa kuelekea uchaguzi mkuu, kwani wanaweza kukikosesha ushindi.
0 comments:
Post a Comment