Na.Semvua Msangi,Dar es
Salaam.
Licha ya kupazwa sauti kila uchao juu ya matukio
ya ajali na mwendo kasi kwa miongoni mwa madereva yanayo tokea na kupelekea
kupoteza maisha ya watanzania wasio na hatia na kuwaacha na ulemavu wa kudumu
lakini bado sauti zinazopazwa zinaonekana sikitu vile kutokana Madereva hao
kuendelea kufanya mashindano wakati wakiwa wamebeba abiria.Hali hii inajitokeza tena leo ambapo Ajali iliyohusisha gari kubwa la mizigo yani SCANIA,na gari ndogo Toyota Rav4,kutokea katika barabara ya Mandela Tabata Relin jijini Dar es Salaam wakati mwenye gari ndogo kujaribu kukwepa Daladala linalofanya safari zake ubungo Temeke wakati likiwa kwenye mwendo kasi nahivyo kusababisha ajali.
Mashuhuda wa ajali wanakiri
kuwa mwenye Daladala alikuwa yupo mwendo kasi jambo ambalo alilipita gari ndogo
mbele wakati kunagari kubwa lilikuwa likitokea nyuma yake hali iliyomlazimu
mwenye gari ndogo kuelekeza gari yake upande mwingine wa bara bara pengine ili
kunusuru maisha yake na ndipo gari hiyo kubwa ikaliginga gari hilo dogo ubavuni
na daladala iliyosababisha ajali ilitokomea baada ya kutambua ilifanya mako.
Wasamaria wema walitoa msaada wakulinasua gari dogo na kubwa ambapo zoezi hilo lilifanikiwa na hivyo kuwacha kila mmoja kuendelea na shughuli zake.,hata hivyo hakuna aliyekufa dhidi ya gari hizo kuwepo na majeraha ya hapa na pale.
Wasamaria wema walitoa msaada wakulinasua gari dogo na kubwa ambapo zoezi hilo lilifanikiwa na hivyo kuwacha kila mmoja kuendelea na shughuli zake.,hata hivyo hakuna aliyekufa dhidi ya gari hizo kuwepo na majeraha ya hapa na pale.
0 comments:
Post a Comment