Image
Image

Adebayor apumzishwa ili kutatua mzozo wa kifamilia.


Mchezajii wa klabu ya Tottenham Emmanuel Adebayor amepewa mapumziko kwa mara ya pili msimu huu lakini hatma yake katika klabu ya Spurs haijulikani. 
Mchezaji huyo wa taifa la Togo mwenye umri wa miaka 31 ameandika kuhusu matatizo ya familia yake katika mtandao wa facebook na kusema kuwa alikuwa ameamua kujiua. 
Adebayor Amekosa mechi ya jana jumapili kati ya kilabu yake na Everton mbali na ziara ya Kuala Lumpur na baadaye nchini Sidney. 
kocha wa kilabu hiyo Mauricio Pochettino amesema wamempa mda wa kusuluhisha mzozo na familia yake. Amesisitiza kuwa hayo ni maisha yake binafsi. Amesema aliongea naye mapema wiki iliyopita na kwamba hiyo ni hali ngumu kwake. 
Adebayor alijiunga na klabu ya Spurs mwaka 2011 kutoka Manchester City kupitia mkopo kabla ya mabao 18 aliyofunga akiwa na Hotspurs kumwezesha kupewa mkataba wa kudumu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment