Image
Image

Kenya kuwashtaki watuhumiwa 29 wa makosa ya ufisadi


Kenya inapanga kuwapandisha kizimbani maofisa 29 wa umma wanaokabiliwa na mashtaka mbalimbali ya ufisadi baada ya kutolewa mapendekezo na Mkurugenzi wa Mwendesha Mashtaka wa Umma.
Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi Halakhe Waqo amesema hadi sasa maofisa 19 wa umma wamefunguliwa mashtaka baada ya kuanzishwa tena mapambano dhidi ya ufisadi miezi miwili iliyopita.
Tume hiyo leo itawasilisha kwa Mwendesha Mashtaka wa Umma nyaraka za mawaziri wanne waliosimamishwa kazi na rais mwezi Machi, ili kutoa fursa ya kufanyika uchunguzi. Bw. Waqo amesema tume imekamilisha uchunguzi wa nyaraka 56, ambapo 21 kati ya hizo zimeshapelekwa kwa Mwendesha Mashtaka wa Umma. Tume imesema maofisa hao wa umma wataondolewa mashtaka baada ya madai dhidi yao kuchunguzwa na kuonekana hawana makosa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment