Akizungumza na Mwanaspoti jana Ijumaa, Bocco alisema
ni lazima ianzishwe kampeni ya kuboreshwa kwa viwanja na yeye yupo tayari
kutumia hata fedha zake kwa nauli ili kuhamasisha jambo hilo.
“Ushauri wangu wa kwanza tunaomba tuanze kampeni ya
kurekebisha viwanja vinavyotumiwa kwa mechi za Ligi Kuu Bara, mimi najitolea
hata mikoani nitaenda kwa nauli yangu mkitaka nisaidieni kwa hilo,”
alisema Bocco.
Bocco alisema angependa kampeni hiyo ianze mapema
kabla ya kuanza kwa ligi ya msimu ujao ili mambo yawe mazuri kabla ya
kugeukia matatizo mengine yanayokwanza soka la Tanzania.
“Lazima tuanze mapema hili jambo, tuna viwanja
vichache kwa ajili ya Ligi Kuu, vingine havifai na vimekuwa vikiwakwaza
wachezaji na timu kwa ujumla, TFF lazima iamke mapema,” alisema Bocco.
Aidha Bocco aliweka hadharani maoni yake sababu ya
Taifa Stars kufanya vibaya kwa miaka mingi na kuwasononesha Watanzania, usome
waraka wake katika ukurasa wa tano.


0 comments:
Post a Comment