Image
Image

Rwanda kujadili katiba yake na namna ya kumuwezesha Rais Paul Kagame kugombea muhula wa tatu.


Bunge la Rwanda litajadili kubadilisha katiba ya  nchi hiyo ili kumuwezesha Rais  PAUL KAGAME kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi utakaofanyika mwaka 2017.
Kwa mujibu wa afisa mmoja katiba ya Rwanda hairuhusu muhula wa tatu kwa hiyo itahitajika katiba ibadilishwe ili kumruhusu.
Maafisa wamekanusha vikali kwamba Bwana KAGAME mwenyewe ndiye anataka muhula wa tatu bali anatakiwa kubaki kwa madai ya watu ya kuleta utulivu na maendeleo ya uchumi wa nchi humo.
Mjadala huo unaotarajiwa miezi miwili ijayo umekuja baada ya Bunge kupokea hoja iliyotiwa saini na watu milioni mbili au asilimia 17 ya idadi ya watu wa nchi hiyo kuomba katiba ibadilishwe kumruhusu Bwana KAGAME kugombea muhula wa tatu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment