Waziri Chikawe ameeleza hayo
baada ya kupokea taarifa ya ujio wa wakimbizi na kutembelea kambi ya muda
katika uwanja wa lake tanganyika mjini kigoma, ambapo amesema serikali
inafuatilia kwa karibu changamoto zilizojitokeza kufuatia ujio wa wakimbizi,
ambapo katibu tawala wa mkoa wa kigoma mhandisi John Ndunguru ameeleza kuwa
kijiji cha kagunga sasa kiko huru baada ya wakimbizi wote kusafirishwa lakini
kinakabiliwa na tatizo la njaa, uharibifu wa mazingira, ugonjwa wa kipindupindu
na uharibifu wa miundombinu.
Kwa upande wake mratibu mkazi umoja wa
mataifa nchini Alvaro Rodriguez ameishukuru serikali ya tanzania kwa kukubali
kuwapokea raia hao wa Burundi ambao wamekimbia machafuko katika nchi yao na
kwamba jumuia ya kimataifa kwa kushirikiana na mashirika yanayotoa huduma kwa
wakimbizi itaendelea kusaidia ili kuhakikisha wakimbizi na jamii ya watanzania
inakuwa salama
Home
News
News Alert:Wakimbizi waliomba hifadhi kutoka nchini Burundi kufanyiwa uchunguzi na SERIKALI ya Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment