Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo JUMA NKAMIA,kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii alipokuwa akijibu swali la Mbunge ANASTANZIA WAMBURA aliyetaka kujua lengo namba tano la Milenia
serikali imefanikiwa kwa kiasi gani.
NKAMIA amesema ni kweli kuwa lengo
namba tano la malengo ya maendeleo
ya milenia ni kupunguza vifo
vya wanawake vinavyotokana na uzazi
kwa robo tatu kuanzia mwaka 2000
hadi mwaka 2015.
Amesema jitihada mbalimbali
z imefanyika ili kupunguza idadi
ya wanawake wanaofariki dunia kutokana na matatizo
ya uzazi ikiwa ni pamoja na mpango mkakati wa kuongeza kasi ya kupunguza
vifo vitokanavyo na uzazi ,watoto wachanga pamoja na
watoto chini ya miaka mitano wa mwaka 2008–2015 .
0 comments:
Post a Comment