Serikali imesema ili kukabiliana na ajali za barabarani lazima abiria wakubali polisi kufanya
ukaguzi wa vyombo vyao vya usafiri pindi
askari anapoona kuna haja ya
kufanya hivyo na siyo kuwatukana na
kuwatoleea kauli chafu pindi wanapojaribu kuwasimamisha kwa lengo la kufanya ukaguzi .
Hayo yamesemwa na
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ,PEREIRA AME SILIMA alipokuwa akijibu
swali la Mbunge wa Kibaha Mjini,SILIVESTER
KOKA,aliyetaka kujua ni taratibu gani zinazotakiwa kufuatwa na pande zote
zinazohusika na ajali.
Naibu Waziri amesema tara tibu za sheria za kushughulikia makosa ya usa lama barabarani ni zile zinazotumika
katika kushugh ulikia makosa
mengine ya jinai .
A mesema iwapo usalama wa maisha ya dereva utakuwa hatarini,dereva anapaswa
kujisalimisha katika kituo cha polisi
cha karibu pamoja
na kutoa ta a rifa
ya ajali hiyo na kuongeza kuwa sheria ya usalama barababani inaeleza kwamba iwapo ajali inahusisha majeruhi dereva analazimika kutoa
taarifa zake na za
mmiliki wa gari kwa askari au mlinzi wa amani aliyepo karibu.
0 comments:
Post a Comment