Baada ya mauaji ya kiongozi wa upinzani Zedi Feruzi
Jumamosi Jioni, vyama vya siasa na mashirika ya kiraia yanayopinga muhula wa
tatu wa rais Pierre Nkurunziza yamechukua uamzi wa kusitisha mazungumzo na
serikali, na kutoa wito kwa wafuasi wao kuanzisha maandamano tangu leo
Jumatatu.
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa umehakikisha kwamba
mazungumzo yataendelea, suala la muhula wa tatu wa rais Nkurunziza kwa sasa
halitakiwi kuwekwa mezani, kwani rais huyo hana haki ya kuwania muhula wa tatu,
amesema kiongozi wa shirika linalopiga vita ufisadi wa mali ya umma Olucome,
Gabriel Rufyiri, mmoja kati ya wanaharakati wanaopinga muhula wa tatu wa rais
Nkurunziza.
Wajumbe wa vyama vya siasa vya upinzani wamesusia
kikao cha mazungumzo cha Jumapili Mei 24 kiliyofanyika kwenye makao makuu ya
Tume ya uchaguzi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi (Minub). Mazungumzo ambayo
yanafanyika kwa wiki tatu sasa.
Hata hivyo wawakilishi wa mashirika ya kiraia
wanaopinga muhula wa tatu wa rais Nkurunziza wameshiriki kikao hicho cha
mazungumzo. Lakini Jumapili jioni wameapa kutorodi kushiriki mazungumzo hayo,
na hivyo kususia wito uliyotolewa na Makanisa Katoliki na Protestanti wa
kuongeza siku moja kwa muda wa siku mbili wa usitishwaji wa maandamano
uliyotangazwa na mashirika ya kiraia na upinzani, muda ambao ulimalizika
Jumapili jioni Mei 24.
Wajumbe wa vyama vya kiraia wametoa masharti ili
waweze kurejea kwenye meza ya mazungumzo ikilinganishwa na hali ya usalama
inayojiri wakati huu.
" Kwanza, tunaomba kuwepo na uchunguzi wa kina
uliyo halali kuhusu mauaji ya Zedi Feruzi, na waliohusika na mauaji hayo. Kwa
njia hiyo, [viongozi] wengine wanaweza kuwa na imani na usalama wao, kwa sababu
wakati huu hatuna usalama wowote ", amesema Gabriel Rufyiri, mwanaharakati
wa vyama vya kiraia.
Watu zaidi ya ishirini wameuawa tangu maandamano ya
kupinga muhula wa tatu wa rais Nkurunziza yaanze wiki nne zilizopita.


0 comments:
Post a Comment