Uongozi wa All Progressives Congress (APC) unailaumu
utawala uliopoa sasa kwa ukosefu mkubwa wa mafuta ukosefu wa umeme na upungufu
wa uzalishaji kutokana na migomo inayoendelea ya wafanyikazi na deni kubwa la
taifa.
APC inailaumu PDP kwa kuiwacha taifa hilo katika
hali mbaya ya kiuchumi na hivyo kuhujumu utawala unaotarajiwa kushika hatamu
karibuni.
Kwa mujibu wa msemaji wa APC Lai Mohammed,''hii
ndiyo mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa serikali kupeana mamlaka
huku uchumi ukiwa katika hali mabaya zaid''
''Kwa sasa uchumi wetu ambao ndio mkubwa zaidi
barani Afrika unadeni kubwa la dola milioni 60 nao wafanyikazi wamegoma wakidai
mabilioni ya fedha.
''Umeme haupo na mafuta pia ambayo ndio nguzo ya
uchumi haipo kwa kweli uchumi umekwama''aliongezea Lai.
Kwa upande wache chama cha rais anayeondoka Goodluck
Jonathan PDP kimekanusha madai ya kuhujumu uchumi wa Nigeria.
Msemaji wa rais Goodluck Reuben Abati,aliwashukuru
wanigeria kwa kumpa fursa ya kuwaongoza .
Kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter alituma
ujumbe kwa niaba ya rais Goodluck ambaye alihudhuria misa yake ya mwisho akiwa
rais na akawaaga wafuasi wao.
Msemaji wa chama chake Olisa Metuh naye aliwaonya
wanachama wa chama cha Buhari kukoma kuichafulia jina chama cha PDP.
Bwana Metuh alisema si kweli kuwa PDP kimehujumu
uongozi na uchumi wa Nigeria
'' Imekuwaje kuwa katika utawala wa rais Goodluck
hakujatokea ukosefu kama huu wa mafuta na umeme ''?
''Nahisi kama kuna watu wenye ushawishi katika
serikali inayokuja ambao wanataka kuzua hali ya taharuki na kuibua madai kuwa
hawakurithi kitu chochote katika akiba ya serikali''.
Mwandishi wa BBC aliyeko Nigeria anasema kuwa chanzo
cha uhaba huo mkubwa wa mafuta na umeme ni mashirika na makampuni yanayoagiza
mafuta ambayo yameamua kususia kuingiza mafuta yakidai malimbikizo ya pesa
wanazodai serikali
enerali mstaafu Buhari alishinda uchaguzi wa urais
wa Nigeria katika uchaguzi uliofanyika tarehe 28 mwezi Machi na kuipa chama cha
upinzani ushindi wake wa kwanza katika historia ya taifa hilo.
Buhari ameratibiwa kuchukua uongozi wa taifa hilo
lenye utajiri mkubwa wa mafuta ijumaa ijayo.
Majuzi kampuni zinazotoa huduma za simu zilitangaza
kuwa zimelazimika kutumia mafuta kuzalisha umeme hatua ambayo ni ghali na kuwa
hazingemudu gharama zake.
Nigeria ambayo huzalisha takriban mapipa milioni
mbili ya mafuta kila siku haina vinu vya kusafishia mafuta nchini humo na
inalazimika kuagiza mafuta kutoka nje.
BBC.




0 comments:
Post a Comment