Image
Image

China yaitaka Philipines iache vitendo vya uchokozi.


Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema, hivi karibuni Philippines inafanya vitendo vya uchokozi katika suala la Bahari ya Kusini, na kusisitiza kuwa China haifanyi ubabe dhidi ya nchi ndogo, lakini nchi hizo pia hazipaswi kufanya uchokozi bila msingi wowote.
Kauli hiyo inatokanana habari kuwa, rais Benigno Aquino wa Philippines jana alisema ndege za Philippines zitaendelea kufanya doria katika sehemu yenye mvutano katika bahari ya Kusini, na China haipaswi kunyanyasa nchi ndogo. Bibi Hua Chunying anasema,
"Nahisi baadhi ya watu wa Philipines wanapiga kelele na kufanya uchokozi juu ya suala la bahari ya Kusini. China imeweka wazi msimamo wake. Nataka kuwakumbusha watu wa Philipines kwamba, China haiwezi kufanya ubabe dhidi ya nchi ndogo, lakini pia tunaona kuwa nchi hizo ndogo hazipaswi kufanya uchokozi bila kusita na bila msingi wowote. Tunaitaka Philipines iache vitendo hivyo, na kurudi kwenye njia ya mazungumzo ili kutatua suala lililopo."
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment