Akizungumza na waandishi wa habari wakati
wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam waziri wa mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa Mh.Bernad Membe amesema kutokana na jaribio la
mapinduzi lililofanyika nchini burundi hivi karibuni kikao kilichopita kiliamua
wakutane tena ili kujadili suala hilo.
Aidha amesema mbali na kupokea taarifa hizo
wanasheria wakuu wa afrika mashariki watatoa taarifa kuhusu uamuzi wa mahakama
ya katiba ya burundi juu ya rais pierre nkurunziza kugombea kwa mara ya tatu na
baada ya kuunganisha taarifa zote hizo ndipo wataziwasilisha kwa marais hao.
0 comments:
Post a Comment