Mheshimiwa LOWASSA aliyewahi kuwa waziri
mkuu wa Tanzania ametoa ahadi hiyo katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha, alipotangaza nia yake ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kimteue
kuwania nafasi hiyo, kupitia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka
huu.
Amesema Tanzania ina rasilimali nyingi na
kinachohitajika ni uongozi imara wa kutokomeza umasikini na kwamba nia yake ni
kuimarisha kusimamia utekelezaji wa sera zilizo bora ili kuchochea maendeleo ya
watu yatakayosimamiwa na serikali ijayo.
Aidha,amesema akipewa nafasi hiyo ya juu nchini atahakikisha
anadumisha muungano.anaweka misingi
imara ya kuharakisha maendeleo na,atawawezesha vijana kuondoa na tabaka
la walionacho nawasionacho.
Amesema kwa vyoyote vile hiyo haiwezi kuwa
kazi ya mtu mmoja ni kazi ya pamoja , hata hivyo anayeongoza timu lazima awe na
mwongozo unaomuongoza.
0 comments:
Post a Comment