Wakimbizi
hao zaidi ya elfu hamsini wanaohifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu wilayani
Kasulu, wametoa ombi hilo wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mheshimiwa MATIAS CHIKAWE katika kambi ya wakimbizi ya Nyaguru wilayani Kasulu
kujionea hali halisi.
Wamesema
mambo yanayoendelea nchini Burundi yako kinyume cha katiba na makubaliano ya
amani yaliyofikiwa Arusha takriban miaka kumi iliyopita, hivyo wakati umefika
sasa wa jumuia za kimataifa kuchukua hatua ili kusitisha uchaguzi kupisha
mazungumzo ya kutafuta muafaka.
Kwa
upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi Mheshimiwa MATHIAS CHIKAWE
amewataka wawe watulivu, wafuate sheria na taratibu wakati huu ambapo jitihada
za kuwahamishia kambi nyingine zikiendelea huku marais wa nchi za Afrika
Mashariki wakiendelea kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi.
0 comments:
Post a Comment