Mwenyekiti huyo wa NEC ametoa
kauli hiyo katika ziara ya kukagua uandikishaji
wa daftari hilo mkoani Dodoma ambapo akiwa wilayani Chemba anakanusha madai
kuwa zoezi hilo linasuasua na kuwataka wananchi katika mikoa ambayo haijafikiwa
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.
Wakati jaji Lubuva akitoa
kauli hiyo wakazi wa baadhi ya maeneo yaliyopitiwa na zoezi hilo la
uandikishaji bado wanaendelea kulalamikia uendeshaji wake ambapo inawalazimu
kutumia mpaka siku tatu kwenye foleni bila mafanikio huku wakihofu kukosa haki
yao ya kikatiba ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Kwa upande wao baadhi
viongozi wa siasa ambao wamekuwa wakitoa hamasa kwa wananchi kujiandikisha
wameiomba serikali kuongeza muda wa uadikishaji hasa kwenye maeneo ambayo yana
idadi kubwa ya watu ili kila mwenye sifa za kujiandikisha apate haki hiyo.
0 comments:
Post a Comment