Bwana Zeid amekaribisha
jitihada za Muungano Afrika, mkutano wa kimataifa wa maziwa makuu, Jumuiya wa
Afrika Mashariki, Muungano wa Ulaya na Umoja wa Mataifa katika kutatua mzozo
huo kwa kuheshimu haki za binadamu, akisema anatumai baraza hilo litatoa ujumbe
mkali ili kusitisha ghasia kwa kuwa…
"Wakati wa ziara yangu
nchini Burundi mwezi uliopita, nimeshtushwa na ukatili wa wanamgambo wa
Imbonerakure, ambao wanaunga mkono serikali ya Rais Nkurunziza. Wanasiasa wa
upinzani, waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za binadamu na kwa kusema
kweli raia wengi wa kawaida bado wanahofia maisha yao."
Halikadhalika, katika hotuba
yake, Kamishna Mkuu ameipongeza Tunisia kwa kufanikiwa katika wakati wa mpito
na kuridhia sheria mpya kuhusu haki za binadamu.
Aidha amezungumzia tatizo la
uhamiaji barani Ulaya na Asia Kusini, akisema lazima kipaumbele kiwekwe katika
kutunza haki za wahamiaji hao kwa kuwaokoa baharini, kuwapatia hifadhi na
kupambana na ubaguzi.
Hatimaye Kamishna Zeid
ameeleza wasiwasi wake juu ya hali ya raia wanaokumbwa na ukiukaji wa haki za
binadamu nchini Sudan Kusini, huku mapigano yakiendelea.


0 comments:
Post a Comment