Wakati dunia imeadhimisha
siku ya kutokomeza fistula duniani Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu
UNFPA, katika ripoti yake limesema kwamba takriban wanawake milioni 2 katika
bara la Afrika, bara Asia na ukanda wa Uarabuni na Amerika ya kusini na Caribea
wanaishi na majeraha na kuna visa kati ya 50,000 hadi laki moja kila mwaka,
licha ya kwamba fistula inaweza kuzuiliwa.
UNFPA imesema uwepo wa ugonjwa huo
ni ishara ya doa katika mifumo ya afya katika kukabiliana na mahitaji ya wanawake.
Kampeni ya kutokomeza fistula
iliyozinduliwa na UNFPA na wadau mwaka 2003 sasa iko katika mataifa ya bara
Afrika na kwingineko ambako Uganda ni moja ya nchi zilizoadhimisha siku hii.
Basi ungana na John Kibego
kutupatia yaliyojiri katika maadhimisho hayo nchini Uganda.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment