Zaidi ya kaya 20 za wakazi wa kitongoji cha mjini
kati na nyabikondo kata ya matongo wilaya ya tarime mkoani mara zimeanguka na
baadhi yake kupata nyufa kufuatia mlipuko mkubwa wa baruti uliotokana na
shughuli ya ulipuaji wa miamba.
Katika tukio hilo watu watatu Jenipher Otiso,
Paschal Marwa na diwani wa viti maalum katika halmashauri ya wilaya ya tarime
Philomena Marwa Tontora wamejeruhiwa na mlipuko huo na kukimbizwa katika
hospitali ya sungusungu iliyopo nyamongo kwa huduma ya kwanza kabla ya
kuhamishiwa katika hospitali ya rufaa bugando jijini mwanza.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiwemo waathirika wa
tukio hilo wamelalamikia hali hiyo kwa madai kwamba kazi ya ulipuaji wa miamba
inapaswa kufanyika baada ya wananchi kupewa tahadhari.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyabikondo Ryoba Magoko
pamoja na mwenyekiti mwenzake wa kitongoji cha mjini kati Mwita Stephen Waigama
wamethibitisha kuanguka kwa nyumba hizo na kueleza madhara yanayoendelea
kuwakumba wananchi wa vitongoji hivyo kwa wakati huu.
Meneja ufanisi wa mgodi wa ACACIA NORTH MARA ambaye
pia ni mwanasheria wa kampuni hiyo Abel Yiga kuhusiana na malalamiko ya wakazi
hao ambapo amesema watu 150 kati ya 1800 wamegoma kuchukua fidia ya malipo yao
kiasi cha shilingi bilioni 23 na kwa hali hiyo wataendelea kukumbwa na mlipuko
wa baruti unaofanyika katika mgodi huo.
0 comments:
Post a Comment