Katika hospitali ya ST
KIZITO MIKUMI walikolazwa majeruhi wa tukio hilo wamesema bomu
hilo lilirushwa na vijana wawili baada ya kutiliwa shaka na
wananchi wa kijiji cha msolwa ujamaa kata ya sanje tarafa ya mangula kuwaweka chini
ya ulinzi kwa ajili ya kuwapekua ambapo vijana hao walirusha bomu na
kujeruhi wananchi pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwa kwenye
gari ya mweneyekiti wa halmashauri wakitokea katika maadhimisho ya mei mosi
ambapo wameomba jeshi la polsi kufanya uchunguz kufuatia
matukio yanayoashiria ugaidi kuendelea kuandama wakazi wa
kilombero.
Nao viongozi wa kata akiwemo diwani wa kata ya
sanje David Ligazio wamesema ipo haja ya serikali kuongeza nguvu ya jeshi la
polisi ikiwa ni pamoja na magari ya usafiri na kutafuta vifaa vinavyo weza
kuchunguza maeneo ya milima ya udizungwa na Ruaha ambapo
wamebaini wahalifu wengi wamewaona wakitokea katika
misitu hiyo mara kw amara.
Kamanda wa polisi mkoa wa
morogoro Lenard Pual amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo
amesema hadi sasa jeshi la polisi linawatafuta watuhumiwa hao ambao
baada ya kurusha bomu hilo limejeruhi dereva wa mweneyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya kilombero na kuharibu gari ya halmshauri
pamoja na wananchi wa kijiji cha msolwa ujamaa.
Tukio hilo limetokea
ndani ya siku 14 baada ya watuhumiwa 9 kukamatwa msikitini wakiwa na
milipuko 30, sare za jeshi, bendera nyeusi pamoja na vitu mbalimbali vya
kufanyia uhalifu huku mmoja akichomwa moto na wananchi wenye hasira akiwa
katika harakati za kutoroka baada ya kumchoma askari kwa jambia shingoni katika
tarafa ya kidadu wilayani kilombero.
0 comments:
Post a Comment