Akizungumza na mamia ya wafanyakazi wa
taasisi,mashirika ya umma na sekta binafsi katika sherehe za maadhimisho ya
siku ya wafanyakazi duniani kwa mkoa wa dar es salaam, mkuu wa mkoa wa dar es
salaam, Bwana Saidi Mecky Sadiki amesema serikali inaelewa matatizo ya
mishahara midogo ya wafanyakazi na mazingira magumu ya kazi na kuwataka
kujituma zaidi na kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa tija badala ya kuwa
wakosoaji na nadharia nyingi.
Awali akizumgumza katika sherehe za maadhimisho
hayo,mratibu wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani mkoa wa dare es
salaam Bwana Charless Mgashi licha kusisitizwa swala la kuongezwa kima cha
chini cha mshahara,amesema wafanyakazi wanataka kupunguzwa kwa kodi katika
mishahara hadi asilimia 9 pamoja na kuondolewa kwa kodi katika mafao ya
wastaafu.
Wakizungumza katika sherehea hizo, badhi ya
washiriki wa wamekuwa na matumani ya serikali
kuongeza kima cha chini cha mshahara iwapo serikali ya mkoa utapeleka
maombi hayo kwa Rais Kikwete,huku wengine wakilalamikia ushirikishwaji mdogo wa
sekta katika sherehe hizo.
0 comments:
Post a Comment