MADAGASCAR imetinga robo fainali ya Cosafa baada ya
kufanikiwa kumaliza vinara wa kundi B wakiipiku Swaziland kwa idadi nzuri ya
magoli ya kufunga na kufungwa.
Timu hizo ambazo zilizokuwa zinachuana kusaka timu
moja ya kutinga robo fainali zimetoka sare ya 1-1 usiku huu.
Mechi ya kwanza ya kundi hilo, Madagascar walishinda
2-1 dhidi ya Lesotho, mechi ya pili wakaifumua 2-0 Tanzania ‘Taifa Stars’ na
leo wametoka sare ya 1-1 na Swaziland.
Kwa matokeo hayo Madagascar wamefunga magoli 5 na
kufungwa 2.
Kwa upande wa Swaziland wao walianza michuano kwa
kuifunga 1-0 Taifa Stars, wakashinda 2-0 dhidi ya Lesotho na leo wametoka sare
ya 1-1 na Madagascar, hivyo wamefunga magoli 4 na kufungwa 1.
Kwa matokeo hayo, mei 24 mwaka huu Madagascar
watacheza mechi ya robo fainali dhidi ya Ghana uwanja wa Moruleng majira ya saa
9:00 kwa saa za Afrika kusini sawa na saa 10:00 kwa saa za Afrika mashariki.
Mechi nyingine ya robo fainali siku hiyo
itawakutanisha Malawi na Msumbiji.
Kwa upande wa kundi A, Namibia walifuzu robo fainali
na watachuana na Zambia mei 25 mwaka huu uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace
majira ya saa 11:30 kwa saa za Sauzi sawa na saa 12:30 kwa saa za Tanzania.
Mechi nyingine ya robo fainali siku ya jumatatu
itawakutanisha wenyeji Afrika kusini dhidi ya Botswana.


0 comments:
Post a Comment