Manjoo amesema mazungumzo
hayo ya wazi yanapaswa kukabiliana na changamoto kama vile unyanyapaa wa kijamii
na ukimya unaoambatana na aina fulani za ukatili, mazingira yasiyojali au
wakati mwingine yasiyokuwa rafiki pale suala la ukatili dhidi ya wanawake
linapotajwa, pamoja na kutoripoti, au kuripoti kwa kiwango cha chini visa vya
ukatili na takwimu haba.
Mtaalam huyo ametaja pia
desturi za kijadi, kitamaduni na kijamii ambazo huzuia kuripoti na kutafuta
usaidizi kutoka kwa watu wasio jamaa wa wahanga wa ukatili, zikijikita kwa
maridhiano badala ya uwajibikaji pale uhalifu unapotendwa dhidi ya wanawake na
wasichana.
Ametoa wito kwa serikali ya
Sudan na wadau wote kutafuta njia ya kufanya mazungumzo yatakayoondoa utata
uliopo, hususan na jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa, kwa maslahi ya watu
wa Sud.
0 comments:
Post a Comment