Akiongea na wataalamu wa
madini kutoka Kituo cha Madini cha Kusini na Mashariki mwa Afrika SEAMIC, Rais
Kenyatta amewataka wahakikishe kuwa nchi za Afrika hazifanyi ubadhirifu
kutokana na ushirikiano na mataifa mbalimbali yachimbayo madini katika bara
hilo. Amesema kwa muda mrefu Afrika imekuwa ikiruhusu rasilimali zake
zimilikiwe na watu wengine, na kusisitiza kuwa sasa wakati umefika wa kuleta
mabadiliko.
SEAMIC ni Shirikisho la
kimataifa lilipo chini ya Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa katika Afrika,
ambayo ilianzishwa mwaka 1977. Nchi wanachama wa shirika hilo ni Kenya,
Tanzania, Uganda, Ethiopia, Sudan, Msumbiji, visiwa vya Comoro na Angola.
0 comments:
Post a Comment