Hii ni kwa mujibu wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, ambalo limesema leo kwenye
taarifa yake kwamba idadi ya watu wanaokumbwa na ukosefu wa usalama wa chakula
imeongezeka maradufu tangu mwanzo wa mwaka huu nchini Sudan Kusini.
Mwakilishi wa UNICEF nchini
Sudan Kusini, Jonathan Veich, amesema licha ya jitihada za UNICEF za kuwasaidia
watoto karibu 50,000 walioathirika na utapiamlo mwaka huu pekee, bado maisha ya
wanawake na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, bila huduma za chakula na
afya, yako hatarini.
Halikadhalika, UNICEF imesema
mapigano kwenye maeneo ya Upper Nile yamesababisha angalau watu 100,000
kukimbia makwao, wakitelekeza akiba zao za mazao na mifugo yao, huko baadhi ya
mashirika ya kibinadamu yakilazimika kuondoka.
UNICEF imetoa wito wa dola
milioni 25 ili kufadhili mradi wake wa kupambana na utapiamlo Sudan Kusini.
0 comments:
Post a Comment