Ripoti hiyo ya hali ya
usalama wa chakula duniani kwa mwaka 2015, imechapishwa na Shirika la Chakula
na Kilimo, FAO, Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD na Shirika la
Mpango wa chakula, WFP.
Ripoti inasema kuwa kuenea
kwa lishe duni, ambacho ni kipimo cha idadi ya watu wasioweza kupata chakula
cha kutosha ili kuwa na maisha yenye afya, kumepungua katika maeneo
yanayoendelea hadi asilimia 12.9 ya idadi ya watu, ikiwa imeshuka kutoka
asilimia 23.3 miaka ishirini na mitano iliyopita.
Nchi 72 kati ya 129
zilizofuatiliwa na FAO zimetimiza lengo la milenia la kupunguza kuenea kwa
lishe duni kwa nusu ifikapo mwaka 2015, huku maeneo yanayoendelea yakishindwa
kutimiza lengo hilo kwa kiwango kidogo mno.
Ripoti hiyo pia inasema kuwa
matukio ya majanga ya hali ya anga, majanga ya kiasili, misukosuko ya kisiasa
na mizozo imezuia kupiga hatua katika baadhi ya nchi, zikiwemo nchi 24 za
Afrika ambazo sasa zinakumbwa na tatizo la njaa. Pietro Gennari, ni Mkurugenzi
wa Idara ya Takwimu katika FAO
“Tuna kundi la nchi
ambazo tumetambua kuwa zimekuwa katika migogoro ya muda mrefu, ambazo
hali zao zinafanana: nchi ambazo zimepigwa na matatizo, zina kiwango cha chini
cha uhimili na kiwango cha juu cha kutokuwa na usalama wa chakula. Matatizo
haya ya nje ama ni maafa ya asili au maafa yaletwayo na mwanadamu. Nchi hizi
kwa ujumla zimekuwa na mafanikio madogo sana katika kupunguza njaa. Nchi pekee
miongoni mwa nchi hizi zenye matatizo ya muda mrefu ambayo imeweza
kufikia lengo la MDG's ni Ethiopia
0 comments:
Post a Comment