Kwa mujibu wa mashuhuda wanadai kuwa mwendesha
Bodaboda ameonekana kutaka kuwahi hivyo kujipenyeza katikati ya magari hayo
hali ambayo imekuwa tofauti na kujikuta akitaka kuyaweka maisha yake rehani kwa
kile wanachoamini kuwa ajali hizi hutokea kutokana na ukiukwaji wa sheria za
usalama Barabarani na kuto tii sheria bila shruti kama kitengo cha usalama Barabarani
ambavyo wamekuwa wakisisitiza mara kwa mara,Magari mawili hayo yakionekana
kuharibika.
Licha ya kutokuwa na mtu yeyote kupoteza maisha
lakini mwendesha Bodaboda huyo ameonekana kuwa na majeraha mbali mbali katika
sehemu za viunga vya mwili wake,ambapo ajali hiyo imesababisha foleni kwa muda
mrefu kidogo.
Tambarare Halisi imeshuhudia askari wa kikosi cha
usalama Barabarani akiendelea na majukumu yake na hivyo kuamua kuyaweka
pembezonui mwa Barabara magari hayo pamoja na Bodaboda hiyo kwa lengo la
kuepusha msongamano wa foleni uliokuwepo hapo.
Tukio hili linatokea baada ya Jeshi la Polisi
kitengo cha usalama Barabarani kuzindua kampeni ya kutokomeza wimbi la ajali za
barabarani ambalo limekuwa likisababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu
kujeruhiwa,na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pindi
wanapoona kanuni na sheria za barabarani zinakiukwa na madereva wazembe.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mohamed Mpinga
wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha usalama barabarani
ijulikanayo zuia ajali sasa,toa taarifa mapema ambayo imeshirikisha kituo cha ITV na Radio One na kushirikiana na
Vodacom pamoja na jeshi hilo amesema matukio ya ajali yatapungua endapo
madereva wote watazingatia kanuni na sheria za usalama barabarani.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika kituo
kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa Radio One Sterio
Deogratius Rweyunga amesema lengo la kituo cha ITV na Radio One ni kuhakikisha
madereva hasa wanaobeba abiria na kwenda masafa marefu wanakuwa makini wawapo
barabarani na kutii sheria ili kunusuru maisha ya watu na kutaja namba za kutoa
taarifa za mienendo mibaya ya madereva ambayo ni 0800757575.
Baadhi ya madereva wa mabasi ya mikoani walieleza
sababu kadhaa zinazochangia ajali za barabarani ikiwemo ubovu wa miundombinu
pamoja na abiria wenyewe ambao wamekuwa wakiwachochea kuongeza mwendo kwa madai
ya kucheleweshwa wanakokwenda huku wakitishia kuhama kampuni ya basi husika
kutokana na dereva kwenda mwendo mdogo.
0 comments:
Post a Comment