Madereva na mabango
Baadhi ya madereva wa mabasi yaendayo mikoani wakiwa nje ya ofisi yao wakiwasikiliza viongozi wao (hawapo pichani).
Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es salaam asubuhi ya leo kusimamia usalama kufuatia mgomo wa madereva wa mabasi ulioanza leo kwa mara nyingine kushinikiza kutekelezewa matakwa yao.
Mabasi yanayofanya safari zake kati ya Dar es salaam na mikoa ya kusini yakiwa yameegeshwa kwenye kituo cha Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es salaam katika mgomo wa madereva leo Hadi muda huu hakuna basi lililoanza safari kutokea kituoni hapo.
Kituo cha Daladala cha Mbagala Rangi Tatu kikiwa kimefurika abiria kufuatia mgomo unaoendelea.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva nchini, Rashid
Saleh akiwatuliza madereva wenzake wakati wakiusubiri Uongozi wa juu wa
Serikali waliotaka kuzungumza nao juu ya matakwa yao waliyoomba wafanyiwe, pindi
walipokutana na Serikali majuma kadhaa yaliyopita.
0 comments:
Post a Comment