Image
Image

News Alert:Rais Kikwete amemteua Balozi Liberata Rutageruka Mulamula kuwa Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Balozi Liberata Rutageruka Mulamula kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sasa Balozi Mulamula ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico.
Rais Kikwete pia amemteua Balozi Hassan Simba Yahya kuwa naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  Kwa sasa Balozi Yahya ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizarani hapo.
Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2015
…………Mwisho…………
Imetolewa ;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
4 Mei, 2015
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment