BUKOBA.
Mamia ya abiria wamekwama
katika standi ya mabasi mjini BUKOBA na kushindwa kusafiri kufuatia
mgomo wa medereva uanaoendelea kufukuta kote nchini na kusabisha adha
kubwa kwa abiria huku wakiendelea kutaabika bila msaada
wowote.
Katika stendi ya mabasi mjini
bukoba ambapo imeshuhudia mabasi yakiwa yamepaki bila kuondoka huku
abilia wakiwa wamelundikana katika stendi hiyo huku
wakiiomba serikali kuchukua hatua za kisheria kwaajili ya
kutatua mgomo huo ambao unaendelea kufukuta hapa nchini na kuleta
adha kubwa kwa wanchi.
Madereva wa basi hayo
walipotea na kutoonekana kabisa katika stendi hiyo ya mabasi bukoba
ambapo mwenyekiti wa taboa mkoa wa kagera Zuberi John
amezungumza kwa njia ya simu ambapo amesema mgomo huo si
wa TABOA ni mgomo wa madereva na TABOA haihusiki katika hilo
nakuongeza kuwa madereva hao wamegoma wakilalamikia hawanamikataba
na kulikataa agizo laserikali la kwenda kusoma kila baada ya miaka mitatu na
kuwatupia lawama madereva kuanzisha mgomo huo bila kuwatangazia abiria mapema
ili wasikate tiketi za kusafiri.
TABORA.
Abiria mkoani TABORA waliokwama
zaidi ya masaa kumi katika standi kuu ya mjini humo, wameitupia lawama serkali
wakidai kuwa, kutosikiliza madai ya wananchi katika idara husika kumekuwa
kukiathiri shughuli za kijamii na kudumaza maendeleo.
Wakizungumza katika stendi
kuu ya mabasi yaendayo mikoani kutokea TABORA, waliokwama tangu alfajiri
wananchi hao wamesema kuwa, migomo hiyo inaathiri mambo mbali mbali, na hata
wakati mwingine kusababisha vifo kama kuna mgonjwa aliyepewa rufaa kwenda
katika hospitali za nje ya TABORA.
Kufuatia mgom huo ambao
haujulikani mwisho wake jeshi la polisi limeweka ulinzi mkali katika stendi
hiyo, ambapo kamanda wa polisi mkoani TABORA kamishina msaidizi SUZANI KAGANDA amesema
kuwa, kwa namna moja ama nyingine wanaweza kujitokeza uhalifu na kusababisha
vurugu katika stendi hiyo kwa lengo la uporaji.
MTWARA.
Zaidi ya abiria 600 waliokuwa
wasafiri kwenda jijijini dar es salaam na wilayani mkoani MTWARA wamekwama kwenye
kituo kikuu cha mabasi mjini humo kufuatia mgomo wa madereva wa mabasi
uliofanyika nchini nzima kama njia ya kuishinikiza serikali kusikiliza madai
yao.
Mgomo huo umeonekana
kuwahusisha pia madereva wa daladala ambapo hakuna daladala zinazosafiri kwenye
barabara za manispaa ya mtwara/mikindani na kuwafanya wafanyakazi na wananchi
wengine walikuwa wakienda mjini kufuata huduma kulazimika kutembea kwa miguu
umbali mrefu kuyafikia maeneo yanayotoa huduma hizo.
Baadhi ya abira hao wameitaka
serikali kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu madai ya madreva hao, kwa kuwa
kinachoonekana ni kuwapa mateso abiria wakiwemo watoto na akina mama.
Kwa upande wao madereva wa
mabasi hayo hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kila mmoja akidai wao sio
wasemaji wa makapuni ya mabasi hayo, hata hivyo abiria walirudishiwa nauli zao
kwa kuelezwa hakuna tena safari .
MSAMVU.
Madereva wa mabasi katika
kituo cha mabasi MSAMVU mjini MOROGORO wamesema hawatakubali kusafirisha abiria
kama serikali haitashughulikia madai yao huku abiria wakiendelea
kukwama katika kituo hicho.
Abiria hao wametupia lawama
serikali kutoshughulikia madai ya madereva ili kuondoa adhaya na
ukosefu wa usafiri kwa wananchi ambapo wamesema mgomo huo umesababisha kukwama
kwa shughuli mbalimbali za kijamii na uchumi.
MBEYA.
Mkoani MBEYA abiria wamepata adha kubwa ya usafiri baada
ya madereva wa magari ya kwenda mikoani, wilayani na yale yanayotoa huduma
katikati ya jiji kugoma, hali ambayo pia imeathiri maisha na shughuli za kila
siku za kiuchumi JIJINI MBEYA.
Mgomo wa madereva ambao
umeanza tangu saa 12:00 asubuhi ukihusisha magari yote ya kusafirisha abiria
umeutikisa mkoa wa mbeya kutokana na mamia ya abiria kushindwa kuendelea na
safari zao, huku wananchi pia wakikwama kuendelea na shughuli zao.
Baadhi ya abiria
wamelalamikia usumbufu ambao wameupata kutokana na mgomo huo na wameitupia
lawama serikali kwa kushindwa kuzuia mgomo huo ambao unafanyika kwa mara ya
pili ndani ya muda mfupi, licha ya kwamba madai ya madereva ni ya muda mrefu.
Katibu umoja wa madereva njia
ya tunduma ambaye pia ni katibu msaidizi wa chama cha madereva kanda ya nyanda
za juu kusini, TANDIZA EDWIN CHIBONA amesema kuwa kwa sasa madereva hawana
imani na viongozi wengine wa serikali na kwamba hatma ya mgomo huo itapatikana
tu baada ya waziri mkuu, mizengo pinda kufikia makubaliano na madereva, huku
akisema kuwa ili kuepuka usanii wa viongozi ni lazima makubaliano hayo pia yawe
katika maandishi na yawekwe kisheria.
Dar
es Salaam.
Mgomo wa mabasi ya abiria na daladala umeitikisa
nchi kwa mara nyigine baada ya madereva wa mabasi na daladala kugoma kwa madai
kuwa serikali imeshindwa kushughulikia madai yao ya msingi.
Katika jiji la Dar es Salaam Tambarare Halisi
imefika kituo kikuu cha mabasi ubungo na kushuhudia msongamano mkubwa wa mabasi ya abiria pamoja na madereva
wa mabasi na daladala wakiwa ndani na nje ya kituo hicho huku polisi nao wakiwa
na silaha za moto, mbwa pamoja na mabomu ya machozi wakiwa wameimarisha ulinzi
nje na ndani ya kituo hicho.
Majira ya asubuhi kamanda wa polisi kikosi cha
usalama barabarani nchini, BW MOHAMMED MPINGA alidai kuwa jeshi la polisi
halina namna ya kutatua mgogoro huo na kwamba baadhi ya viongozi wa madereva
wanakwenda kuonana na waziri mkuu Mh.MIZENGO PINDA.
Hata hivyo chama cha wamiliki wa mabasi nchini Tanzania
TABOA wao wamesema hawaungi mkono mgomo
huo wa madereva na hawakupata taarifa mapema ndio maana wakaendelea na zoezi la
kukatisha tiketi huku wakiitaka serikali kutoa muongozo wa mgogoro huo mapema
ili kuepusha athari zaidi ambazo zinaweza kutokea.
Mwenyekiti wa vyama vya madereva CLEMENCT MASANJA baada ya kumtafuta kupitia njia ya simu ya
mkononi amedai kuwa viongozi wa madereva wameshindwa kwenda kuonana na waziri
mkuu kutokana na madereva hao kuzingira ofisi zao na kuwazuia wasiende wakitaka
waziri mkuu huyo kufika kituo hicho cha mabasi na kuzungumza nao iwezekanavyo
ili kujua hatima na mtizamo wa serikali juu yakile wanacho shinikiza.
Aidha Katika mazungumzo na waandishi wa habari
wakati waziri wa uchukuzi akitangaza hatua zilizochukuliwa na serikali ikiwemo
waziri mkuu kuunda kamati ya kudumu ya kushughulikia madai ya madereva hao,
waziri huyo amelalamikia kitendo cha madereva hao kukataa wito wa waziri mkuu,Kufuatia
mgomo huo katika maeneo mbalimbali ya
jiji idadi kubwa ya abiria wameonekana wakitembea kwa miguu nyakati za asubuhi na
jioni huku baadhi ya wanafunzi, madereva na abiria wamesema kuwa hali hiyo
sinzuri kwao na hata kwa taifa kuonekana na kuwa na sura tofauti ya
migomo,jambo ambalo wanaamini wakikaa pamoja na kutekeleza huenda nchi ikabaki
salama na migomo ikawa historia.
Baadhi ya wananchi wengine wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa
itafikia wakati watu watachoka na hivyo nchi kuingia katika machafuko na hivyo
hata kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na suala ambalo
lingemalizika kwa maafikiano lakini linachukua muda kumalizika.
Wamesema machafuko yanayotokea katika nchi za
wenzetu hayapendezi kuyaona yakirindima nchini humu ikiwa kuwa Tanzania ni
kisiwa cha amani huku wakitolea mfano namna Burundi hali si shwari hadi
wakimbizi wanaingia nchini mwetu na kuwapokea na wao kujisikia amani sasa
nasisi tukiingia katika machafuko nani wakumfuta mwenzake machozi,Jibu bado
nikitendawili.
0 comments:
Post a Comment