Image
Image

News Alert: Serikali kushusha viwango vya kodi ya ardhi mwezi julai mwaka huu ili kuondoa migogoro ya ardhi.

Serikali imetangaza kushusha kuanzia tarehe mosi mwezi julai mwaka huu viwango vya kodi ya ardhi na gharama za upimaji ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengi kuwa na ardhi iliyopimwa hali itakayonchangia kuondoa migogoro iliyokithiri ya ardhi hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI katika kikao cha baraza kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo ambapo amekiri kuwa gharama za ardhi ni kubwa na mara zote wananchi wa kawaida hawana uwezo wa kulipa na kuchangia kuwepo migogoro ya ardhi isiyo ya lazima.

Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa wizara ALPHAYO KIDATA aliwataka watendaji wa ngazi zote wanohusika na masuala ya ardhi kuzingatia weledi na miiko ya kazi kufuatia sekta ya ardhi kunyooshewa vidole kwa utendaji mbovu kila kukicha.

Kwa upande wao washiriki wa baraza hilo wamekiri migogoro mingi ya ardhi ambayo mingine inasababisha hata kuwepo matukio ya vifo na umwagaji wa damu ambayo yanachangiwa na baadhi ya maofisa wa ardhi na changamoto ambazo zimekuwa zikichangia migogoro ya ardhi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment