Ni sehemu ya wakazi wa eneo hilo la
vikongoro wakipaza sauti zao mara baada ya ITV kufika eneo la tukio kushuhudia
kilichotendeka ambapo wakazi hao wamesema wamevunjiwa nyumba zao pamoja na zile walizokuwa wakiendelea
kujenga ilhali wanamiliki maeneo hayo kihalali.
Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo EFESO MSEMO amesema vijana
waliohusika na kufanya uvunjaji huo
walikuwa wakichukua vitu walivyokuwa
wakikuta ndani ya nyumba hizo sambamba na kunywa vinywaji walivyokuwa wakikuta
katika maduka wanayoyavunja.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ameiambia ITV kwa njia ya simu
kuwa alipewa taarifa na kamanda wa polisi wa wilaya ya kipolisi ya ukonga kuwa
uvunjaji huo unatokana na wakazi hao kuvamia katika eneo ambalo linamilikiwa
kihalali na mtu mwingine.
Source:ITV.
0 comments:
Post a Comment