Wakizungumza kwa huzuni wananachi wa vijiji
vya kitete na kadudu wameeleza mvua
zimesababisha madhara makubwa ikiwemo nyumba kuanguka na
kusababisha baadhi ya kaya kukosa makazi
ambapo kwa sasa wananchi hawana
chakula kutokana na vyakula kuharibika baada ya kujaa maji huku mazao yaliopandwa mashambani yakiwemo
mahindi yameseombwa na mvua na kuomba serikali kuwasaidia chakula
wanachi waliokubwa na mafuriko.
Akitoa tarifa za tathmini ya awali ya mafuriko
hayo afisa tarafa wa tarafa ya dumila MOSES
NCHIMBI amesema nyumba zilizo anguka kabisa
ni nane na nyingine 80 zimeharibika vibaya na kujaa maji ambapo ameeleza chanzo cha athari hizo hayo ni kuziba kwa mto DYONGOYA
kutokana na baadhi ya wananchi kulima kando ya mto huo.
Mkuu wa wilaya ya kilosa BWANA JOHN NJEWELE
amewapa pole wananchi wa vijiji hivyo kwa athari walizozipata ambapo ameagiza watendaji wa vijiji kata na
vitongoji kuanza zoezi la kukagua na
kubaini wananchi waliolima na kujenga kando kando ya mito
na kusabaisha mito kuziba na maji kupoteza uelekeo na kujaa katika
makazi ya wananchi.
0 comments:
Post a Comment