Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya misenyi FADHILI
NKURLU katika hafla ya kupata chakula cha mchana na watu
wenye ulemavu wa ngozi albino wilayani misenyi ambapo amesema
mwalimu atakae thubutu kumfukuza mtoto mwenye ulemavu
waongozi albino au mtoto wa mtu mwenye ulemavu kwa kumdai gharama yoyote
shuleni atachukuliwa hatuka akali za kisheria.
Mapema akiongea katika hafla hiyo mwenyekiti wa
chama cha albino mkoa wa kagera BUCHARD EMMANUELI ameeleza
changamoto na misukosuko ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo kwa
kuhofia kuwawa huku akiomba serika kuwapatia gharama za usafili ili
waweze kufika katika mkutano mkuu wa kimataifa wa siku ya albino
duniani utakao fanyika jijini Arusha kwaanzia tarehe tisa mwezi wa
sita na kuhakikisha ulinzi unaimarisha ili waweze kuishi kwa amani kama watu
wengine.
Katika hafla hiyo watu wote wenye ulemavu
wa ngozi albino wa wilaya ya misenyi walipatiwa bima za afya
kwaajili ya kupata matiba bure bila gharama yoyote pamoja na simu za mkononi
kwaajili ya kutoa taarifa kwenye mamlaka husika pindi watakapo kuwa
wana watilia mashaka watu wasiowema wanaotaka kuhatarisha maisha
yao.
0 comments:
Post a Comment