Viongozi wanne wa serikali
kuanzia ngazi za vijiji na kata wilayani kilindi wametiwa mbaroni na jeshi la
polisi baada ya kubainika kuhusika na uvunaji haramu wa misitu ya asili kisha
kusafirisha magogo na mbao kwenda ndani na nje ya nchi.
Akizungumza ofisini kwake
baada ya sakata hilo,mkuu wa wilaya ya kilindi Bwana Selemani Liwowa amesema
viongozi hao ni kutoka kata za kimbe na mkindi pamoja na watendaji wao ambao
kwa pamoja wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi
kisha kuhujumu hifadhi za misitu iliyopo katika kata zao.
Hata hivyo baadhi ya
wafanyabaishara wenye leseni halali waliokuwa wakivuna misitu ya mashamba ya
watu binafsi wamelalamikia kuwa kitendo walichofanya cha kukaatwa na
kuwekwa mahabusu ni cha udhalilishaji kwa sababu wameingia
mikataba na serikali za vijiji ili waweze kuvuna misitu ya asili iliyopo
katika mashamba ya watu binafsi kwa ajili ya kutengeneza madawati na zahanati
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya taifa ya kusaidia shughuli za
maendeleo.
kufuatia hatua hiyo wadau wa
biashara za mbao waliopewa leseni na wakala wa misitu na nyuki kanda ya
kaskazini wamelalamikia kitendo cha wao kukamatwa na kuwekwa mahabusu kisha
kudaiwa kuwa wanaleseni za kughushi hatua abayo wameahidi kulifikisha
katika vyombo vya sheria kupitia wakili wao ili waweze kudai fidia walizolipa
kwa serikali zaidi ya shilingi milioni 100.
0 comments:
Post a Comment