Image
Image

News Alert: Wakimbizi toka Burundi wamiminika Tanzania kupitia Kigoma



Na Editha Karlo
Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wakiwasili nchini kwa boti hivi  maeneo ya Kibirizi, Mkoani Kigoma. Bado idadi yao haijafahamika kwani bado zoezi la kuwaandikisha linaelea katika eneo hilo. 

Ujio wa waomba hifadhi hawa unakuja kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Burundi  ambayo yameshika kasi na kusababisha wananchi kuanza kukimbilia nchini Tanzania.
Burundi ilikumbwa na machafuko katika miaka ya nyuma na baadaye kuwa na amani lakini sasa inaingia katika mgogoro tena baada ya Rais wa sasa Pierre Nkurunzima kutaka kuwania urais kwa muhula mwingine.

Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wakijiandikisha mara baada ya kuwasili nchini Tanzania leo kwa boti.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment