Image
Image

News Alert: Wananchi wa TEGETA wafunga barabara ya BAGAMOYO na kuwaamuru watu wenye magari binafsi kubeba wanafunzi kufuatia mgomo wa madereva unaondelea nchi Nzima.


Jeshi la polisi mkoa wa kipolisi kinondoni jijini Dar-es-salaam,wakiongozwa na kamanda wa polisi wa mkoa huo ACP CAMILIUS WAMBURA,limelazimika kuingilia kati kwa kuondoa mawe na viroba vya mchanga,vilivyokuwa  vimemewekwa barabarani na baadhi ya wananchi wa TEGETA waliofunga barabara ya bagamoyo,na kuwalazimiasha madereva wa magari madogo kubeba wanafunzi kufuatia mgomo ulioitishwa na madereva nchini nzima.

Tambarare Halisi  imeshuhuduia tukio hilo lililodumu kwa dakika kumi kabla ya jeshi hilo kutawanya wananchi hao hasa vijana,bila ya kutumia nguvu ya ziada na magari kuanza kupita lakini wananchi hao wakiwa vikundi vikundi na polisi kulazimika kuweka kambi katika eneo hilo la kituo.

Hali hiyo ikavuta hisia na umati wa watu wengi kuja kushuhudia haswa kile kilichojiri eneo hilo ambapo hali ya usafiri imekuwa ya kuogofya kutokana na daladala zifanyazo safari kuacha kufanya safari kwa siku hii ya leo ambapo ukipita baadhi ya maeneo magari hukuta yakiwa yamepaki pembeni huku yakionyesha ishara yakutofanya kazi kwa siku hii ya leo endapo madai yao ya msingi hayatasikilizwa na kufanyiwa kazi kwa wakati.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment