Serikali imewaondoa hofu wakazi wa Kigamboni kuwa hawataondolewa katika maeneo yao na
badala yake waliopo kwenye maeneo ambayo miundombinu muhimu inapita
watafidiwa.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba
na Maendeleo ya Makazi , ANJELA KAIRUKI
alipokuwa akijibu maswali
mbalimbali ya wabunge
Amsema endapo wananchi hawatakuwa na mitaji
wataingia ubia na wenye nayo na pale watakaposhindwa wataweza kuuza maeneo yao
au watalipwa fidia.
Baadhi ya wabunge wakati wanauliza maswali ya
nyongeza wameitaka Serikali kueleza ni lini Serikali itaelekeza maafisa ardhi
nchini kupima maeneo ya umma , zikiwemo
shule na hospitali , ambayo yamekuwa na migogoro ambayo wakati mwingine inaweza
kusababisha uvunji f u wa amani.
Na kuhusu tatizo la majengo kuporomoka , kutokana na madai ya vifaa vinavyotumika
kutokuwa na viwango ama kujengwa chini ya kiwango , Waziri KIGODA amesema ili kudhibiti tatizo
hilo Shirika la Viwango Tanzania - TBS
- imekuwa ikihakikisha bidhaa
zote zinazozalishwa nchini zinakidhi kiwango cha kimataifa cha bidhaa husika.
0 comments:
Post a Comment