Kamati hiyo itakutana Jumatatu wiki ijayo kufanya tathimini ya hali itakavyoendelea kuwa nchini humo
na kuona nini kifanyike,kwani
mpaka sasa haijajulikani ni nani
anayeongoza nchi hiyo kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais PIERE NKURU
NZINZA na wanajeshi waluiofanya
mapinduzi .
Mwenyekiti wa mawaziri hao ambaye pia ni Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania,BERNARD MEMBE
amesema ,kwa hali ilivyo hivi sasa nchini Burundi zin ahitajika jitihada za
ziada kwa kila mpenda maendeleo,ili
kunusuru vurugu zinazoendelea nchini
humo .
Kuhusu mahali alipo Rais PIERE NKURUNZINZA Waziri
MEMBE amekataa kutaja mahali alipo
kiongozi huyo wa Burundi.
Ingawa uchunguzi unaonyesha kuwa Rais huyo mara baada ya kuondoka na ndege jana kurudi Burundi nakushindwa kuhudhuria kikao cha EAC baada ya kupata taarifa za kupinduliwa na Jeshi hakuweza kufika baada ya kuwekewa vizuizi kufuatia amri ya Meja jenerali wa Jeshi Godefroid Niyombare kuamuru taa za uwanja wa ndege kuzimwa na kutoruhusiwa Ndege yeyote kutua nchini humo ambapo Rais Nkurunzinza Inaelezwa alirudi na yupo hapa jijini Dar es salaam na alilala moja ya hoteli kubwa mjini hapa.

Katika hatua nyingine nalo Baraza la Uslaama la
Umoja wa Matiafa leo hii limeitisha kikao cha dharura kujadili hali ya mambo
Burundi baada ya jenerali mwandamizi jeshini kutangaa kunyakua madaraka kutoka
kwa Rais Pierre Nkurunziza. Kikao hicho cha dharura kimeitishwa na
Ufaransa huku katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitoa wito wa
utulivu na ustahamilivu nchini Burundi. Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unafuatilia
kwa karibu kinachoendelea nchini Burundi na kusisitiza kauli ya Katibu Mkuu Ban
Ki-moon aliyotoa wakati wa mkutano wa viongozi wa Muungano wa Afrika huko Addis
Ababa, Ethiopia kuhusu awamu za uongozi. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja
wa Mataifa Stephane Dujarric aliyezungumza mjini New York, wakati wa mkutano na
waandishi wa habari waliotaka kufahamu msimamo wa chombo hicho kuhusu hali
iliyoripotiwa Burundi.
Jana baada ya kuenea habari Jenerali Godefroid
Niyombare kumpindua Rais Pierre Nkurunziza, rais huyo alijaribu kurundi nchini
kwake kutokea jijini Dar es Salamu, Tanzania alikokuwa amekwenda kushiriki
kikao cha marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC. Hata hivyo ndege
yake ilishindwa kutua baada ya askari watiifu kwa Niyombare, kuzingira uwanja
wa ndege wa Bujumbura. Bado haijabinika Nkurunziza yuko wapi.
0 comments:
Post a Comment