Image
Image

News Alert:Wabunge wamtaka waziri mkuu Pinda kuangalia namna ya ujenzi usiozingatia uhifadhi wa mazingira ili kuwanusuru wakazi waliokubwa na Mafuriko.


Baadhi ya wabunge wa jiji la Dar es Salaam wamemtaka waziri mkuu kuiangalia Dar es Salaam kwa jicho la kipekee hasa katika ujenzi wa miundombinu ya maji ya mvua pamoja na udhibiti wa ujenzi usiozingatia uhifadhi wa mazingira ili kuwanusuru wakazi wa jiji hilo na maafa ya mafuriko ambayo yamekuwa yakiwakumba kila mara na kusababisha vifo.
Kauli hiyo  imetolewa na wabunge wakati wakichangia bajeti ya ofisi ya waziri mkuu na bunge ambapo wamegusia suala la mafuriko katika jiji la da es salaam lililo wafanya watu kupoteza maisha na wengine kukosa makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kubomoka kufuatia mvua iliyonyesha na kusababisha mafuriko.

 Baadhi ya wabunge wametaka kusikia sauti ya waziri mkuu juu ya mafuriko hayo pamoja na kutoa maelezo ya kinaga ubaga  juu ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda sasa na  kusababisha ajali za mara kwa mara wakitolea mfano eneo la Ruvu Kibaha.

Mh.Idd Azan ambaye ni  Mbunge Kinondoni na Mh Zungu Mbunge Ilala,Lucy Owenya Mbunge Viti Maalum Chadema wamekuwa na kiu ya kujua na kufahamu juu ya msimamo wa Mh. Waziri pinda->>Bofya Hapa kuona na kusikia walichouliza.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment